Sunday, 1 February 2015

Zawadi zaongezeka Ngorongoro Marathoni


https://zaratours.files.wordpress.com/2012/04/546761_10150651371547116_545457115_9874508_1106404433_n.jpg
Baadhi ya wanariadha wakichuana katika mbio za Ngorongoro Marathoni mwaka jana.

Na Mwandishi wetu
WAANDAAJI wa mbio za Ngorongoro Marathoni Kampuni ya Zara Charity mwaka huu wameongeza zawadi kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyika Aprili 18, imeelezwa.
Kwa mujibu wa mratibu wa mbio hizo zinazofanyika kila mwaka Meta Petro, washindi wa mwaka huu kwa wanaume na wanawake wote watapata zwadi sawa tofauti na miaka ya nyuma.
Petro alisema kuwa katika mbio za miaka iliyopita, washindi wakiume walikuwa wakipata zawadi zawadi licha ya kukimbia mbio za umbali mmoja kama zile za kilometa 21.
Alisema kuwa lengo la kuongeza zawadi na kuweka viwango sawa ni kuondoa unyanyapaa na kuweka usawa kati ya wakimbiaji wakike na wale wa kiume ambao hukimbia umbali mmoja.
Alitaja zawadi za mwaka huu kwa mshindi wa kwanza kwa wanaume na wanewake ni kiasi cha Sh. Milioni 1.2 kwa watakaokimbia mbio za nusu marathoni, yaani kilometa 21.
Petro alisema kuwa, mwaka jana mshindi wa kwanza kwa wanaume aliondola na kitita cha Sh. Milioni 1 wakati mshindi wa wanawake alipewa kiasi cha sh. 500,000 tu.
Mwaka huu washindi wa pili bila kujali jinsi zao kila mmoja ataondoka na kiasi cha Sh. 600,000 wakati mwaka jana aliondoka na Sh.500,000 kwa wanaume wakati kwa wanawake alipewa Sh. 300,000
Washindi watatu kila mmoja atakabidhiwa kitisha cha Sh. 400,000 huku washindi wa tano hadi wa  10 kila mmoja anatarajiwa kuondoka na kifuta jasho kimono ambacho hakukitaja.

No comments:

Post a Comment