Thursday, 19 February 2015

John Terry anogewa Chelsea
LONDON, England

JOHN Terry anataka kuongeza kuichezea Chelsea kwa miezi mingine 12, imeelezwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 anayechezea nafasi ya beki wa kati, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu, ameichezea timu hiyo mechi 656 katika miaka 16 ya kuwachezea vinara hao wa Ligi Kuu ya England.
"Klabu inajua nafasi yangu, " alisema nahodha huyo wazamani wa England. "Nataka kubaki. Bila shaka kiwango changu kimeonesha na kinaweza kunibakisha.
"Nitafurahi kupata mwaka mmoja na nitaona unaendaje. Naongeza mwaka kwa mwaka. Sina chaguo zaidi."
Terry aliichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo Oktoba mwaka 1998, na alichukua nafasi ya Marcel Desailly kama nahodha wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2004-05.
Ni nahodha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya klabu hiyo, ambapo ameiongoza kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu, mafanikio katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kutwaa mara nne taji la FA na mara mbili lile la Ligi.
Frank Lampard na Ashley Cole ambao ni wachezaji wazamani wa Chelsea waliruhusiwa kuondoka Chelsea mara mikataba yao ilipofikia mwisho.
Kiungo Eden Hazard, 24, ndiye mchezaji wa hivi karibuni kabisa wa Chelsea kusaini mkataba mpya, kitendo kilichoungwa mkoo na Terry, ambaye aliongeza: "Hazard ameshafanya na hicho ni muhimu zaidi kwa klabu. "

John Terry.

No comments:

Post a Comment