*Ataka aendelee kuwa rais
CAIRO, Misri
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Issa Hayatou anataka
kubadili Katiba katika kipengere kinachohusu uko wa umri, ili aweze kugombea
kipindi kingine tena cha uongozi.
Caf katika sheria zake inataka kiongozi aliyefikia umri wa miaka
70 kuachia ngazi lakini mabadiliko yatajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa CAF
mwezi Aprili.
Hayatou,mwenye umri wa miaka 68, anatumikia kipindi cha saba
ofisini, baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998.
"Fifa hawana ukomo wa umri kwa wajumbe wake wa Kamati ya
Utendaji, hivyo Caf nao wanataka kutumia nafasi hiyo kubadili Katiba ili waende
sambamba nao, “alisema
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Caf Kwesi Nyantakyi.
Utawaka wa sasa wa Hayatou unamalizika mwaka 2017 na anasaka miaka
mingine kinne ya kuliongoza shirikisho hilo la soka kwa miaka minne zaidi angalau
hadi mwaka 2021, wakati atakaofikishaumri wa miaka 75.
Kipengere kimoja cha Katiba ya Caf kinasema hivi "wakati wa
uchaguzi wao, wagombea wote lazima wawe wajumbe wa vyama vyao vya soka vya nchi
wanazotoka, wagombea wote wa Kamati ya Utendaji ya Caf lazima wawe wajumbe wa
Kamati ya Utendaji kwa vyama vyao vya soka vya nchi na lazimwawe na umri,
No comments:
Post a Comment