Wednesday, 18 February 2015

Jeshi Nigeria laua Boko Haram 300 
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau akiwa na baadhi ya askari wake.

ABUJA, Nigeria
ZAIDI ya wapiganaji 300 wa Boko Haram wameuawa katika zoezi la kijeshi huko Kaskazini-Mashariki ya Nigeria, limesema jeshi la Nigeria.
Baadhi ya askari wamekamatwa na silaha zimeharibiwa, alisema msemaji wa jeshi Chris Olukolade.
Pia katika tukio hilo askari wawili walipoteza maisha yao na wengine 10 walijeruhiwa wakati wa zoezi hilo la siku mbili huko katika jimbo la Borno, aliongeza.
Hatahivyo, vifo hivyo havukuthibitishwa.
Jeshi la Nigeria lilituhumiwa katika siku zilizopita kuwa limekuwa likitoa taarifa za uongo kuhusu kujeruhiwa kwa maadui.
Boko Haram wamevamia raia huku wakiwaua maelfu wa askari tangu kundi hilo lianzishe vurugu kwa ajili ya kuanzisha taifa lao la kiislamu mwaka 2009.
Nigeria, Chad, Cameroon na Niger hivi karibuni vimeunda jeshi la muungano na kudai kuwa limekuwa likifanya vizuri dhidi ya Boko Haramu.

No comments:

Post a Comment