Friday 6 February 2015

Tunisia yazua jambo Afcon




RABAT, Morocco
WAZIRI wa Michezo na Vijana wa Tunisia, Saber Bouatay, amezitaka Morocco, Algeria, Libya na Misri kuiunga mkono nchi yake na kujitoa katika Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
Shirikisho la Soka la Tunisia limeripoti kuwa kamwe halitaomba radhi kwa Caf kutokana na kitendo chake kabla ya mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya wenyeji Guinea ya Ikweta.
Shirikisho hilo la soka la Afrika liliamua kulipiga faini Shirikisho la Soka la Tunisia dola 50,000 kwa kile ilichokiita kuwa, vitendo na tabia zisizokubalika vilivyofanywa na viongozi na wachezaji wake.
Caf lililiomba shirikisho la soka la Tunisia kuandika barua ya kuomba radhi kwa madai waliyotoa kuwa timu yao haitatendewa haki.
Pia shirikisho hilo la soka la Tunisia limeambiwa litaongezewa adhabu endapo halitawasilisha barua mapema.
Kamati ya Nidhamu itaishauri Kamati ya Utendaji ya CAF kuhusu kuongezewa adhabu kwa Tunisia, ikiwemo ya kutokubali ushiriki wa nchi yao hiyo katika fainali zijazo za Mataifa ya Afrika, Afcon za mwaka 2017,ilisema Caf katika taarifa yake.

Tunisia walipinga dhidi ya mwamuzi kutoa penati ya utata kwa wenyeji Guinea ya Ikweta katika muda wa majeruhi na kuwasaidia kuvuzu kwa raundi inayofuata.
Wenyeji Guinea ya Ikweta walifanikiwa kupata bao jingine ambalo liliwawezesha kutinga fainali.
Rais wa Shirikisho la Soka la Tunisia Wadie Jary alijiuzulu katika Caf bkatika harakati za kumpinga mwamuzi huyo liyetoa penati ya utata kwa wenyeji.
Hatahivyo, CAF ilimfungia mwamjuzi huyo wa Mauritiuan , Rajindraparsad Seechurn, kwa kipindi cha miezio sita kwa kushindwa kumudu mchezo.
.

No comments:

Post a Comment