Wednesday, 25 February 2015

Vazi lamwangusha Madona stejini akitumbuiza


Nyota wa muziki wa Pop Madona akianguka stejini wakati akitmbuiza.
LONDON, England
NYOTA wa muziki wa pop Madonna jana alijikuta akipiga mweleka katika steji wakati akitumbuiza katika hafla ya utoaji tuzo za Brit 2015.
Muimbaji huyo alipiga mweleka kutoka jukwaa na kuangukia mgongo baada ya mcheza shoo wake mmoja kuvuta `shela (mfano wa kofia ndefu aliyoivaa kutoka kichwani) mwanzoni mwa onesho hilo.
Hatahivyo, mwanamuziki huyo mkongwe alikuwa fiti na alirejea tena stejini na kumalizia kibao chake, `Living For Love.
Baadae mwanamuziki huyo baadae alitoa taarifa rasmi na kusema
kuwa "yuko fiti" na `shela lake hilo lilikuwa limebana saa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwishoni mwa hafla hiyo ambayo Ed Sheeran na Sam Smith wote walishinda tuzo.

No comments:

Post a Comment