Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao. (Picha na Maktaba) |
Na Seba Nyanga
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Azam FC, leo wamerejea
kwa kishindo katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo baada ya kuichapa Mtibwa
sugar kwa bao 5-2 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Chama Complex
Mbagala Dar es Salaam.
Mabao mawili ya Frank Domayo na washambuliaji Kipre Tchetche na
Didier Kavambagu, aliyefunga moja, yamewapa uongozi wa ligi hiyo Azam FC
wakifikisha pointi 25 sawa na Yanga SC waliowafunga Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo imeshuhudiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi
Mart Nooij aliyekuwa Jukwaa Kuu la Uwanja huo wakati Mtibwa Sugar ikipokea
kipigo hicho cha aina yake.
Azam FC imefunga mabao 22 na kufungwa 12 wakati Yanga wamefunga
mabao 15 na kuruhusu mabao saba.Kila timu imecheza jumla ya mechi 13.
Vikosi
vilikuwa;
Azam FC: Manula, Kapombe, Nyoni/ Bocco (dk.65), Moradi, Wawa,
Bolou/ Mudathir Yahya (dk. 55), Tchetche, Domayo, Kavumbagu/ Mcha (dk.80), Sure
Boy na Majwega.
Mtibwa Sugar
SC:
Said Mohamed, Andrew Vicent, Majaliwa Mbaga, Ally Lundenga/ Vicent Barnabas
(dk. 46), Salim Mbonde, Shaban Nditi, Ramadhani Kichuya, Musa Nampaka, Ame Ally
Amour, Henry Joseph/ Ally Shomari (dk.33) na Musa Hassan ‘Mgosi’ na / Abdallah Juma (dk. 70).
No comments:
Post a Comment