Thursday, 19 February 2015

Ronaldo ni mabao tu-Ancelotti

Cristiano Ronaldo.
MADRID, Hispania
MCHEZAJI Cristiano Ronaldo "maisha yake ni kupachika mabao " kwa mujibu wa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti, aliyempokea mshambuliaji huyo ambaye amerejea katika fomu ya kupachika mabao.
Ronaldo alianza mchezo wa jana Jumatano wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Schalke bila ya bao katika mechi tatu zilizopita, lakini alifunga bao la kuongoza wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo huo wa kwanza.
"Cristiano amerudi," alisema Ancelotti wakati mshambuliaji huyo akifikisha bao la 58 katika mechi 58 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Leo tulikuwa tunahitaji mchezo kama ule, kwa tabia kama hii. Kila kitu kilikwenda vizuri. "
Ancelotti, aliyeiongoza Real Madrid kutwaa taji la 10 la Ulaya msimu uliopita, alielezea kuwa na imani na Ronaldo  wakati wa maandalizi ya mchezo huo baada ya kuulizwa kuhusu ukame wa mabao wa mchezaji huyo.
Mchezo wan ne bila ya kupata bao ilikuwa kipindi kibaya zaidi kwa Ronaldo mbele ya lango tangu mwaka 2011, lakini baada ya dakika 26 alifunga na baadae alitoa pasi kwa Marcelo, aliyefunga katika kipindi cha pili.

"Alifunga, alicheza vizuri na alisaidia kupatikana kwa bao," aliongeza Ancelotti. "Sio tatizo kwetu kama hajafunga mchezo mmoja au miwili ni wazi lile bao limemfanya kuwa vizuri.

"Katika takwimu sio bao tu-bao. Lilikuwa bao zuri la kuongoza,
Bao hilo la kwanza la mchezaji huyo wazamani wa Manchester United katika mwezi lilitoa msingi mzuri kwa Madrid ambayo imeshinda mechi 10 mfululizo za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ikifikia rekodi ya Bayern Munich, waliyoiweka mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment