Sunday, 8 February 2015

Black Energy yang'ara tamasha la Nyama Choma


Mshindi wa shindano maalum katika banda la Brack Energy akipokea zawadi yake ya fulana.


Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Nyama Choma lilifanyika Jumamosi kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wengi, lilifana.
Mbali na nyama choma pia kulikuwepo na burudani mbalimbali viwanjani hapo kuwaburudisha watu waliofika kushuhudia uhodari wa kuchoma nyama kutoka kwa wataalam mbalimbali.
Pia kulikuwa na mabanda mbalimbali ya bidhaa tofauti zikiwemo zile za vinywaji baridi na moto kama Black Energy, Coca Cola, Heniken na vingine vingi.
Hatahivyo, kwa upande wa vinywaji, banda la Black Energy kinywaji ambacho hakina kilevi na chenye kutia nguvu mwilini, banda lake lilitia fora miongoni mwa mabanda ya vinywaji.
Banda hilo lilikuwa na vinywaji vya Black Energy vya aina mbalimbali vikiwemo vile ambavyo havina sukari au Sugae Free Drink ambacho ni mahsusi kwa watu wasiopenda sukari kama wale wagonjwa wa kisukari.
Pia banda hilo lilikuwa na michezo mbalimbali ambapo mshindi alipata fulana au vinywaji vya Black Energy.
Watoto, watu wazima, wanawake kwa wanaume walimimika katika banda hilo ambapo mbali na kupata maelezo ya kinywaji hicho kutoka kwa wahudumu, pia walicheza kuwania zawadi au kununua vinywaji hivyo, ambavyo wengi walivifurahia.

No comments:

Post a Comment