*Ni baada ya vifo kutokea uwanjani sababu ya vurugu
Mashabiki wakizozana na polisi wakati wakitaka kuingia uwanjani. |
CAIRO, Misri
SERIKALI ya Misri imesimamisha mechi za ligi kwa muda usiojulikana
baada ya kutokea vurugu uwanjani na kusababisha vifo vya takribani watu 22.
Watu walipambana baada ya polisi kulipua mabomu ya machozi kwa
mashabiki wa timu ya Zamalek waliokuwa wakilazimisha kuingia uwanjani
kushuhudia mchezo dhidi ya wapinzani wao ENPPI.
Hatahivyo, mashabiki hao walilalamikia wahusika kwa kutumia mlango
mmoja tu hapo uwanjani na kusababisha msongamano.
Hati ya kukamatwa imetolewa kwa viongozi wa kundi la mashabiki wa
klabu ya Zamalek, ambao wanajulikana kama `the White Knights’.
Kwa mara ya mwisho ligi ilisimamishwa mwaka 2012 baada ya
mashabiki 74 kufa wakati wa vurug katika mchezo huko Port Said.
Angalau watu 20 waliumia Jumapili mjini hapa kwenye uwanja wa
Jeshi la Anga, alisema shuhuda mmoja.
Licha ya vurugu hizo, mchezo huo uliendelea.
Uwanjani jozi za viatu viliachwa na watu waliouawa huku majeruhi
wakiwa hoi uwanjani hapo.
Mashabiki wa Zamalek wanadai kuwa vurugu hizo zilianza wakati
viongozi walipofungua geti moja la waya kuruhusu watu kuingia uwanjani.
Mashuhuda hao walisema kuwa ukuta wa waya ulianguka wakati umati
wa watu ukilazimisha kuingia. "Mara askari walianza kulipua mabomu ya
machozi…," alisema
shuhuda mmoja.
No comments:
Post a Comment