MALABA, Equatorial
Guinea
TIMU ya
taifa ya Ivory Coast imemkaribisha kwa mikono miwili katika mazoezi ya timu
hiyo mchezaji wake Cheick Tiote kabla timu hiyo leo haijashuka dimbani
kucheza mchezo wao wa nusu fainali wa
Mataifa ya Afrika.
Ivory
Cioast baada ya kuitoa Tunisia katika
hatua ya robo fainali, inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano
hayo makubwa kwa nchi barani Afrika.
Cheick
Tiote huenda leo Jumatano akawemo katika kikosi cha Ivory Coast cha nusu
fainali dhidi ya Jamhuri ya Watu wa Kongo.
Kiungo
huyo mahiri wa Newcastle United hajapangwa katika kikosi cha kocha wake Herve
Renard tangu alipoichezea timu hiyo kwa
mara ya mwisho wakati ilipocheza na Mali katika mchezo wa Januari 24 kutokaana na maumivu ya kifundo
cha mguu.
Hatahivyo,
kocha wa timu hiyo Renard ana matumaini makubwa kuwa, mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 28, atarejea uwanjani na wanafuzu kwa fainali zao za sita ndani ya
miaka sita katika mashindano hayo.
"Tiote
alianza mazoezi mepesi na yumo katika orodha ya kikosi cha leo Jumatano
kitakachoshuka dimbani.
"Kwa
kweli ni vigumu kwake kuanza mchezo huo, lakini yumo katika kikosi hicho.
Ivory
Coast wanaangalia kutwaa taji lao la kwanza la AFCON tangu mwaka 1992 huko Equatorial
Guinea, huku kocha Renard akiwa na matumaini kibao ya kujaribu bahati ya kulitwaa
taji hilo tena baada ya kufanikiwa kufanya hivyo alipokuwa akiifundisha
Zanzibar mwaka 2012.
Kesho
Alhamisi kutakuwa na nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Ghana na wenyeji
Equatorial Guinea ambao watakuwa wakicheza mbele ya wapenzi wao.
No comments:
Post a Comment