*Lengo ni kuzalisha walimu wenye ujuzi watakaotoa wachezaji bora
Mratibu wa michezo mkoa wa Kinondoni Mwl. Samuel Robert akizungumza Makongo leo kabla ya ufungaji rasmi wa mafunzo ya walimu wa michezo wa shule za sekondari Kinondoni. |
Na Mwandishi Wetu
KANDA ya Kinondoni imekamilisha mafunzo maalum kwa ajili ya walimu
wa shule za sekondari watakaofundisha mikoa yao kwa ajili ya kuiwezesha kanda
hiyo kuendelea kutamba katika mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Kinondoni kwa miaka minne mfuulizo imetamba katika Michezo ya
Umisseta kwa kutwaa vikombe vingi na kuwa mshindi wa jumla wa mashindano hayo
ya kila mwaka.
Mratibu wa michezo Kanda ya Kinondoni mwalimu Samuel Robert amesema
leo kuwa, lengo la mafunzo hayo n
Alisema mafunzo hayo yaliohusisha michezo mbalimbali pia
yatasaidia kuongeza ari kwa walimu hao ili wafundishe kwa utaalam zaidi.
Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha swalimu 30 kutoka shule
mbalimbali za sekondari Kanda ya Kinondoni na yalihusu michezo ya mpira wa
miguu, kikapu, wavu, netiboli, mpira wa mikono na riadha.
Alisema kuwa kila mchezo ulikuwa na walimu watano na ulifundishwa
na wakufunzi walioletwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia vyama au
mashirikisho ya kitaifa ya michezo hiyo.
Mafunzo hayo yalitolewa na wataalam wa kitaifa na kimataifa wa
michezo hapa nchini kama akina Suleiman Nyambui na Mwinga Mwanjala wa riadha,
Manase Zablon wa kikapu na wengine.
Kanda ya Kinondoni kiumisseta wameigawa katika wilaya mbalimbali
za Kawe, Ubungo, Wilaya Maalum ya Makongo na Kinondoni yenyewe.
Naye mkufunzi wa riadha Nyambui aliwataka walimu kuzingatia
mafunzo hayo ili kuchagua wanafunzi wenye sifa watakaokuwa na uwezo wa kufanya
vizuri katika mchezo wa riadha.
No comments:
Post a Comment