Na Mwandishi
Wetu
MBIO
za 13 za Kilimanjaro Marathoni zinafanyika mjini Moshi Machi mosi mwaka huu na
kutarajia kushirikisha wanariadha zaidi ya 800 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kila
mwaka mbio hizo zimezidi kupata umaarufu mkubwa kwa washiriki, wadhamini na
watazamaji kuzidi kujitokeza kwa wingi kila mwaka kutokana na umaarufu wa mbio
hizo.
Mbali
na mbio za kilometa 42, mbio za walemavu na zile za kilometa tano za
kujifurahisha, pia ziko mbio maarufu za nusu marathoni, ambazo zinadhaminiwa na
Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo.
Kwa
mara ya kwanza mwaka huu Tigo watadhamini mbio hizo za nusu marathoni za
Kilimanjaro na watatoa zaidi ya Sh. Milioni 80 kwa ajili ya shughuli mbalimbali
zikiwemo zawadi kwa washindi.
Tigo
kwa kushirikiana na makampuni mengine watadhamini mbio hizo za Kilimanjaro
Marathoni, na
fedha zitakazopatikana kutoka kwenye mashindano
haya zitatumika
kwa ajili ya kulinda mazingira yanayouzunguka Mlima Kilimanjaro.
Zawadi
Kwa Washindi:
Tigo
imetenga kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa ajili ya washindi wa mbio za nusu marathoni. Washindi wa kwanza upande wa wanawake na
wanaume watazawadia Sh.Milioni 2 kwa kila mmoja, na tayari washiriki 5,000
wameshajiandikisha kwa ajili ya kushiriki mbio hizo za nusu marathoni.
Pia
kampuni hiyo itawadhamini wafanyakazi wake watano kwa ajili ya kushiriki mbio
hizo za nusu marathoni.
MVUTO
KWA WASHIRIKI:
Mbio
za Kilimanjaro Marathoni zimeendelea kuwa kivutio kwa washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi,
wanariadha nyota hapa nchini wakiwemo Fabian Joseph, Dickson Marwa, Mary
Naali,Catherine Lange na Jacqueline Sakilu wamethibitisha kushiriki kwenye mbio
za km 21 na pia mwaka huu mbio hizo zinatarajia kushirikisha zaidi ya
wakimbiaji 800 kutoka nchi 40 duniani.
Baadhi
ya nchi ambazo tayari zimethibitisha kushiriki ni pamoja na Marekani, ambayo
italeta wakimbiaji wengi zaidi, ikifuatiwa na Uingereza, Canada, Japan, Uganda,
Zimbabwe, Kenya, Sweden, Australia na Hungary.
Nchi
zingine ambazo zitaleta wakimbiaji wake ni Ujerumani, Sweden, Norway, Italia,
Ufaransa, Japan, China, Zambia, Morocco, Swaziland, Nigeria na Malawi.
Meneja chapa wa Tigo William Mpinga anasema kuwa mbio hizo zinatambulika na Shirikisho
la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) na pia zitatumika kufuzu kwa mbio
rafiki, ambazo ni zile za Oceans na zingine za kimataifa zilizomo katika
kalenda ya IAAF.
Mpinga
anasema kuwa wamefurahi kuwa sehemu ya mbio hizo za kila mwaka ambazo zimekuwa
na mafanikio makubwa na kuvutia watalii wengi kuja kuona Mlima Kilimanjaro, ambao ni alama na kivutio muhimu cha watalii.
Mpinga
alisema mbali na kufurahia mbio hizo za nusu marathoni za Tigo, mashabiki na
wakazi wa Moshi mjini watapata fursa ya kuona na kupata bidhaa na huduma za
Tigo wakati wa masindano hayo.
Kama
kampuni ya kitanzania pia tunajivunia kushiriki katika tukio hili linalovutia
hisia si tu za wanamichezo wengi wa nje, bali
pia ni fursa ya kipekee kuonyesha vipaji vya wanamichezo wa ndani, aliongeza.
UONGOZI
WA RT:
Akizungumza
hivi karibuni jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania(RT) Suleiman Nyambui
anasema kuwa mbio za Kili Marathoni ni mbio kubwa zaidi nchini na maandalizi ya
mbio hizo yako katika hatua za mwisho na kusisitiza kuwa zitashirikisha pia
nyota wa riadha kutoka nje ya nchi
No comments:
Post a Comment