Afcon kuchezwa Novemba 2023
ZURICH, Uswis
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) Jerome
Valcke anasema kuwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2023 zitahamishwa
kutoka Januari kama ilivyokawaida na kuchezwa Juni, ili kufanikisha fainali za
Kombe la Dunia 2022.
Kamati ya Maandalizi ya Fifa imependekeza fainali za
Kombe la Dunia zitakaopigwa Qatar zifanyike Novemba na Desemba ili kukwepa joto
kali mwezi Juni.
"Kamati ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) ni
wazi itaandaa fainali hizo za Mataifa ya Afrika Novemba na Desemba na sio
Januari 2023 kama ilivyozoeleka, alisema Valcke.
***
Serikali yasimamisha ligi Uturuki
ATHENS, Ugiriki
SERIKALI ya Ugiriki imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi
ya kulipwa ya nchi hii kwa sababu ya vurugu, imeelezwa.
Kufungiwa kwa ligi hiyo kumekuja kufuatia vurugu za
Jumampili za mchezo wa Super League kati ya Olympiakos na Panathinaikos, pamoja na ngumi kuzuka miongoni
mwa viongozi wa klabu hizo katika mkutano wa bodi Jumanne.
Tayari ligi hiyo msimu huu ilisimamishwa mara mbili
katika mwezi Septemba na Novemba.
Kiongozi mpya wa chama cha tawala cha nchi hiyo Syriza ameahidi
kukomesha vurugu hizo.
***
Khan awaponda Mayweathe, Pacquiao
LONDON, England
BONDIA Amir Khan anaamini kuwa pambano la wakali wawili
katika ndondi za kulipwa kwa sasa Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao litakalofanyika
Mei 2, halitakuwa na msisimko.
Bondia huyo Muingereza aliponda kwa kusema kuwa
wanamasumbwi hao wawili tayari wakati wao ulikuwa umeshapita, hiyo hawatakuwa
na jipya.
Lakini Mayweather anasema kuwa pambano hilo
litakalofanyika Las Vegas litakata kiu ya wapenzi wa ndondi duniani.
Pacquiao na Mayweather watakutana Mei 2 baada ya muda
mrefu wa makubaliano.
***
Djokovic amsambaratisha Glubev
DUBAI, UAE
MCHEZA tenisi Novak Djokovic alitumia dakika 61 tu
kumsambaratisha Andrey Golubev na kutinga robo fainali ya mashindano ya Dubai
Duty Free.
Djokovic, ambaye ni bingwa mara nne wa mashindano hayo,
kamwe hakumpa nafasi mpinzani wake na kumsambaratisha kwa seti 6-1 6-2 ndani ya
saa moja.
Mchezaji tenisi huyo namba moja kwa ubora katika mchezo
wa tenisi duniani sasa atapambana na Mturuki Marsel Ilhan, ambaye aliyemshitua
anayeshilia nafasi ya sita Feliciano Lopez kwa 3-6 7-5 6-3 aliyeshinda katika
kiwanja namba tatu.
No comments:
Post a Comment