Wednesday 25 February 2015

Ligi Misri kuchezwa bila mashabiki




Polisi nchini Misri akimthibiti shabiki.
CAIRO, Misri
LIGI Kuu ya Misri ambayo ilisimamishwa, itaendelea tena mwezi ujao wa Machi huku wapenzi wa soka wakizuiwa kushuhudia michezo hiyo.
Ligi hiyo ilipigwa stop baada ya kutokea vurugu uwanjani na kuua watu karibu 19 kutokana na vurugu hizo za mashabiki na polisi nje ya uwanja jijini hapa Februari 8 mwaka huu.
Baada ya kikao cha leo Jumatano, baraza la mawaziri la Misri katika taarifa yake lilisema kuwa, ligi inaweza kuendelea "bila ya mashabiki baada ya kumalizika kwa siku 40 za maombolezo ".
Hatahivyo, taarifa hiyo haikusema bayana ni lini hasa ligi hiyo itaanza kuchezwa huku mashabiki wakizuiwa kushuhudia mechi hizo.
Maafa hayo yalitokea kabla ya mchezo kati ya klabu za jijini hapa ya Zamalek na ENPPI wakati polisi na mashabiki walipopambana.
Polisi walilipua mabomu ya machizo na kurusha silaha nyingine kwa mashabiki hao, ambao walikuwa wakilazimisha kuingia uwanjani kushuhudia pambano hilo.
Hiyo iliuwa ni mara ya kwanza kwa idadi maalum ya mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi za ligi tangu Februari 2012, wakati mashabiki 72 wa Al Ahly walipokufa walipokuwa wakipambana na wenzao wa Al Masry kwenye uwanja wa Port Said.

No comments:

Post a Comment