Saturday 7 February 2015

Mabondia 39 kuchuana Uwanja wa Ndani



 *15 bora kuchaguliwa timu ya taifa


Na Seba Nyanga
MABONDIA 39 kuanzia Jumatatu Februari 9 mwaka huu watachuana katika Uwanja wa Ndani wa Taifa kusaka nafasi ya kuchaguliwa katika timu ya taifa itakayoshiriki Michezo ya Mataifa ya Afrika.
Michezo ya Mataifa ya Afrika Septemba 4-19 huko Brazzaville, Congo, na ngumi ni miongoni mwa michezo 21 itakayoshindaniwa katika michezo ya mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), Anthony Mwangonda alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanatarajia mashindano hayo yatakuwa ya kiwango cha juu.
Alisema kuwa BFT imepania kurejesha kiwango cha mchezo huo hapa nchini na mabondia hao walichaguliwa kutoka katika mashindano ya wazi ya taifa yaliyofanyika Uwanja wa Ndani wa Taifa na kufanya vizuri.
Mwangonda ambaye ni bondia wazamani aliyepata mafanikio katika ndondi za ridhaa alisema kuwa, BFT itakuwa makini sana katika mashindano hayo ya mchujo, ili kuwawezesha kupata mabondia bora 15 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo hiyo ya Afrika.
Alisema kuwa kamwe hawatachagua bondia kwa kujuana au kwa kufuata umaarufu wa jina lake, kwani watachagua kutokana na kufanya vizuri katika ndondi hizo za mchujo.
Mabondia watakachuana katika mchujo:-
Lightfly: Ibrahim Abdallah (Magereza), Said Hofu (JKT), Gervas Longasian (Arusha) na Said Stephen (Kigoma).
Fly: Shabani Mnimba (Temeke), Hafidh Mohamed (JKT), Muhsin Kimwaga (JKT)na  Michael Andrew (Temeke).
Bantam: Tuwer Son (JKT), James Star (JKT), Ahmed Furahisha (JKT), Bashir Mkumbula (JKT), Robert Nobert (Kagera) na Hassan Yussuf (Magereza).
Light: Bosco Bakari (JKT), Swahiba Athumani (Arusha), Mohamed Ibrahim (Tanga),  Undule Langson (Magereza), Fidel Castro (Kigoma) na Silaji Kassim (Kagera).
Walter: Victor Njaiti (JKT), Issa Rashid (JKT), Shaban Bruno (Arusha), Kassim Khalfan (JKT) na Babu Buluda (Morogoro).
Lightmiddle: Gulash Rashid (JKT), Seleman Bamtula (JKT) na Mustapha Mtoro (Temeke).
Middle: Ivan Mussa (Kagera), Abuu Said (JKT), Hafidh Mwaipaja (Magereza) na Frank Florian (Kigoma).
Lightheavy: Robert Kyaruz (Kagera), Frank Kawesi (Lindi), Freddy Julius (Kigoma) na Daniel Mwambinga (Magereza).
Heavy: Alex Sitta, Maulid Kitenge na Fabian Gaudence.

No comments:

Post a Comment