Wednesday, 4 February 2015

Caf yamfungia mwamuzi miezi sita



Mwamuzi Rajindraparsal Seechurn akizongwa na viongozi wa timu ya taifa ya Tunisia
CAIRO, Misri
MWAMUZI mmoja wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika amefungiwa miezi sita baada ya `kuchezesha chini ya kiwango.

Rajindraparsad Seechurn aliyewazawadia wenyeji Equatorial Guinea penati ya utata katika muda wa majeruhi wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 2-1 katika hatua ya robo fainali.

Vingozi wa timu ya taifa ya Tunisia walimzonga mwamuzi huyo baada ya mchezo kumalizika na hilo limepelekea Shirikisho la Soka la nchi yao kupigwa faini ya dola 50,000 (sawa na Pauni 33,000).

"Kamati ya Waamuzi ilibaini kutomudu mchezo kwa mwamuzi huyo, yaani kuchezesha chini ya kiwango, " ilisema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

Caf iliongeza kuwa, alishindwa kabisa kuleta hali ya utulivu kwa wachezaji wakati wa mchezo huo ".

Caf pia inataka Tunisia imembe radhi kwa kutoa kauli ya kuituhumu Caf kuwa ilipanga mayokeo.

Na Tunisia imetakiwa mara kufifia uharibifu wa mlango na jokofu katika chumba cha kubadilishia nguo wachezaji kwenye uwanja wa Bata.

Mwamjuzi huyo Muauritian Seechurn alitoa penati katika muda wa majeruhi baada ya Ali Maaloul kulazimisha kuwa alifanyiwa madhambi na Ivan Bolado wakati Tunisia ikiongoza kwa bao 1-0 kupitia kwa Balboa, wenyeji Equatorial Guinea walishinda wakati wa muda wa nyongeza.

Seechurn pia baada ya kufungiwa ameondolewa pia katika orodha ya Caf ya waamuzi.

No comments:

Post a Comment