Kocha Nasoro Sharifu. |
Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya mpira wa wavu wa ufukweni wametamba
kufanya vizuri katika mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika kwa ajili ya kufuzu
kucheza Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani Rio de Jeneiro, Brazil.
Mashindano hayo ambayo mbali na Tanzania pia yatashirikisha Burundi, Djibout, Somali, Kenya na Ethiopia, yataanza kutimua vumbi Jumatatu Februari 16 hadi 18.
Wakizungumza kwa walisema kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi na
wana matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo, ambayo
yatafanyika kwenye ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es
Salaam.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Nasoro Sharifu alisema kuwa mazoezi yanaendelea
vizuri na pamoja na ugeni wa timu ya Tanzania katika mchezo huo, lakini
wanatarajia kufanya vizuri sana.
Everline Alberth |
Naye mchezaji wa kutumainiwa wa Tanzania Prisons Everlyine Alberth
alisema kuwa wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Alisema kuwa pamoja na ugeni wa Tanzania katika michuano ya wavu
wa ufukweni, lakini watafanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa.
Zuhura Jaco wa Jeshi Stars alisema kuwa kuwa wanajiandaa vizuri na
lengo lao kuifikisha mbali Tanzania katika mashindano hayo na wanaomba kuungwa
mkono na mashabiki.
Zuhura Jaco |
Zuhura Jaco wanaendelea vizuri na mazoezi na wana matumaini
makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo muhimu kwa ajili ya kufuzu kwa
Michezo ya Olimpiki.
Hope Agapa. |
Naye Hope Agapa alisema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri
katika mashindano hayo na lengo lao ni kufika mbali ili kuitoa kimasomaso
Tanzania.
Mohamed Ismail. |
Mohamed Ismail alisema kuwa mashindano yatakuwa magumu lakini wana
matumaini ya kufanya vizuri na kufika mbali.
Farhan Aboubakar au Babu |
David Evarist |
No comments:
Post a Comment