Tuesday, 3 February 2015

Chelsea yakamilisha kumnasa Cuadrado
 * Ni jembe la uhakika


LONDON, England
JUAN Cuadrado mekamilisha usajili wake kutoka klabu ya Fiorentina kwenda vinara wa Ligi Kuu ya England Chelsea kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Chelsea ilithibitisha kulinasa jembe hilo Mcolombia Juan Cuadrado kutoka Fiorentina.

Baada ya wiki za tetesi, hatimaye Chelsea ilitangaza rasmi kumnasa mchezaji huyo na aliwasili jana ikiwa ni muda mfupi baada ya kuondoka kwa Andre Schurrle kwenda klabu ya Wolfsburg.

Cuadrado alitumia miaka mitano na nusu kuchezea timu za Italia, kwa muda mfupi alikuwa na Udinese kabla hajakwenda Fiorentina mwaka 2012 baada ya kuwa kwa muda mrefu katika klabu ya Lecce.

"Nimefurahi sana na ninashukuru kwa kupata nafasi hii niliyopewa, " alisema katika mtandao rasmi wa klabu hiyo.

"Hii ni klabu kubwa na ukweli ni kama ndoto vile kujiunga na familia ya Chelsea na unajua kocha ananiamini. Kwa kweli nimefurahi sana."

Cuadrado ana mabao matano katika mechi 37 alizoichezea timu ya taifa ya Colombia, na alikuwa mchezaji tegemeo mwaka jana katika fainali za Kombe la dunia nchini Brazil, kabla timu hiyo haijatolewa katika robo fainali na wenyeji.


No comments:

Post a Comment