Murray arejea katika nne bora
LONDON, England
LICHA ya kushindwa na Novak Djkovic katika mchezo wa wikiendi
iliyopita wa fainali ya mashindano ya Australian Open, Andy Murray amerejea
katika wachezaji wane bora duniani wa mchezo wa tenisi.
Andy Murray amerejea katika nne bora ya viwango vya ubora vya ATP baada
ya kutokuwepo kwa miezi 12, akimaliza wa pili katika mashindano ya Australian
Open Jumapili.
Mscotland huyo aliporomoka kutoka katika nne bora mwaka mmoja
uliopita, huku mara moja tu akifanikiwa kutinga robo fainali ya Melbourne mwaka
2014, lakini amerejea katika nafasi hiyo baada ya kumchapa bingwa namba moja
duniani Novak Djokovic na kumyima taji kubwa la tatu katika historia yake ya
mchezo huo.
Murray alichapwa 7-6 (7-5) 6-7 (4-7) 6-3 6-0 lakini alirejea
katika kiwango chake na kupanda nafasi mbili na kuwa nyuma ya Djokovic, Roger
Federer na Rafael Nadal.
Milos Raonic alikuwa mchezaji mwingine aliyeweza kuboresha kiwango
chake cha ubora kwa nafasi mbili zaidi, akipaa hadi nafasi ya sita baada ya
kutupwa nje na Djokovic katika robo fainali.
Muaustralia Nick Kyrgios alifaidika na mashindano hayo kuchezewa
katika ardhi ya nyumbani kwao baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 19
kupanda hadi nafasi ya 18 kati ya nafasi 35 ikiwa ni mara yake ya pili kucheza
robo fainali ya mashindano makubwa.
Mwenzake Bernard Tomic naye amepoteza nafasi ya 18 hadi kuwa wa 48
wakati Stan Wawrinka aliporomoka kwa nafasi tano hadi wa tisa baada ya
kushindwa na Djokovic katika hatua ya robo fainali na kumzuia kutetea taji
lake.
Kwa upande wa wanawake, Ana Ivanovic aliteleza kutoka nafasi ya
tano hadi ya sita baada ya kushindwa na mchezaji kutoka Jamhuri ya Czech Lucie
Hradecka katika raundi ya kwanza na Caroline Wozniacki aliyepanda nafasi tatu
na kuwemo katika tano bora.
Serena Williams, ambaye hilo ni taji lake la sita la Australian
Open lilimsaidia kuendelea kushika usukani huku dada yake Venus alipanda kwa
nafasi saba hadi ya 11.
No comments:
Post a Comment