Kocha Mkuu wa Mwadui Jamhuri Kihwelo akisisitiza jambo. |
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE timu ya Mwadui FC ya Shinyanga imepanda daraja na msimu
ujao itashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imeelezwa.
Timu hiyo ambayo mwaka jana nusura icheze Ligi Kuu kama sio
kufanyiwa mizengwe, inafundishwa na kocha wazamani wa Simba Jamhuri Kihwelo.
Kupanda kwa Mwadui ni faraja kubwa kwa viongozi wa soka a mkoa wa
Shinyanga kwani sasa mbali na timu hiyo pia kuna timu ya Stand United ambao wanashiriki
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mwandui imepanda daraja baada ya kujihakikishia pointi 43 baada ya
kuikandika Polisi ya Tabora kwa bao 2-0 katika mchezo uliopigwa mkoani
Shinyanga.
Aidha, mchezo mwingine wa kundi B kati ya Toto African ya Mwanza
na Geita Gold SC ulivunjika baada ya kutokea vurugu na mwamuzi kupokea
kichampo.
Toto African ya Mwanza wana pointi 39 wakiwa mbele ya JKT Oljoro
pamoja na Polisi Tabora ambao kila mmoja ana pointi 38.
Mwaka jana Julio alitaka kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu lakini kufuatia
TFF kuchelewa kutoa maamuzi baada ya mchezo wao na Stand United kuvunjika na
kusababisha kutotinga Ligi Kuu na badala yake msimu huu kucheza Ligi Daraja la
kwanza.
No comments:
Post a Comment