*Mahakama yapunguza vipengele vya sheria ya ugaidi
Kenyatta International Conference Centre (KICC). |
Nairobi, Kenya
SERIKALI ya Kenya imepata pigo baada ya Mahakama ya Katiba kuondoa
baadhi ya vipengele katika sheria mpya ya usalama ili kukabiliana na ugaidi.
Muungano wa upinzani nchini Kenya na mashirika mbalimbali yalienda
mahakamani mwaka uliopita baada ya bunge kupitisha sheria hiyo.
Jopo la majaji watano wa Mahakama Kuu wakiongozwa na Jaji Isaac
Lenaola walifutia mbali vipengele 10 kikiwemo kile kinachohusu uhuru wa vyombo
vya habari na haki ya washukiwa wanapofikishwa mahakamani.
Uamuzi huo ulichukua kama saa saa tano na majaji wakaamua kuwa
baadhi ya vipengele havikuaambatana na Katiba.
Katika uamuzi wao walikubali kuwa Kenya imekumbwa na visa vingi
vya ugaidi katika miaka ya hivi karibuni na inastahili kuwa na mbinu za
kuisaidia kukabilana na tatizo hilo.
Majaji hao walisema kuwa haki ya washitakiwa inatakiwa kuzingatiwa
pia.
Mengine yaliyoharamishwa yanajumuisha kuwalazimisha wanahabari
kuchapisha baadhi ya picha kwa ruhusa ya polisi,
kuwazuia washukiwa bila kuwapa nafasi ya kujitetea na kuwanyima
dhamana washukiwa wakipelekwa mahakamani bila sababu zozote.
Aidha, mahakama hiyo imekataa jaribio la Serikali kutaka kuweka
kiwango cha wakimbizi wanaostahili kuhifadhiwa Kenya wazidi 150,000 na kusema
hiyi ni kinyume na mkataba Geneva.
Uamuzi huo wa mahakama umefueahia na Muungano wa upinzani wa CORD.
Hatahivyo, serikali kupitia wakili wake imesema kuwa iko njiani
kukataa rufaa k,upinga uamuzi huo wa mahakama.
Sheria hiyo ilipitishwa Bungeni Desemba 14 mwaka jana katika kikao
kilichotawaliwa na vurugu huku baadhi ya wabunge wakizichapa kavu kavu.
No comments:
Post a Comment