Sunday, 22 February 2015

Nadala achapwa nusu fainali Brazil
RIO de JENEIRO, Brazil
RAFAEL Nadal (pichani) amepoteza nusu fainali ya kwanza ya mashindano yanayochezewa katika katika uwanja wa udongo katika kipindi cha miaka 12 wakati alishindwa na Fabio Fognini katika mashindano ya Rio Open.
Nadal, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni bingwa mtetezi alicheza vizuri lakini alijikuta akichapwa kwa 1-6 6-2 7-5 kwa muda wa saa mbili na dakika 17.
Kipigo hicho cha Brazil kimemaliza ushindi wa mechin 52 mfululizo wa nusu fainali katika mashindano hayo yanayofanyikia kwenye uwanja wa udongo kwa Muhispania huyo.
Muhispania mwenzake David Ferrer atakabiliana na Fognini katika fainali.
"Nimefurahi sana kuhusu mchezo huu. Nimemfunga mchezaji bora kabisa katika dunia hii, " alisema mchezaji huyo Muitalia anayeshikilia namba 28 kwa ubora duniani.
"Rafa siku zote ni mgumu. Kuanzia seti ya pili nilicheza vizuri sana, na nilijaribu kubadili mchezo."


Kwa Fognini huo ulikuwa ni ushindi wake wa kwanza katika majaribio yake matano dhidi ya Nadal, ambaye alionekana wazi amechoka mchezo ulipozidi kuendelea.

No comments:

Post a Comment