Monday 16 February 2015

Wavu wa ufukweni waanza Dar



*Wanawake wa Tanzania waanza kwa ushindi


Wachezaji wa Tanzania Hellen Richard na Everlyine Alberth wakati wa mapumziko walipocheza na Burundi leo.


Farahan Aboubakar (kushoto) na Ismail Mohamed wa timu ya taifa ya Tanzania ya wavu wa ufukweni wakipata kinywaji cha Black Energy baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Burundi. Burundi ilishinda 2-1.Black Energy ndio wadhamini wa timu za Tanzania katika mashindano hayo
Na Seba Nyanga
MASHINDANO ya mpira wa wavu wa ufukweni kwa ajili ya kusaka timu zitakazocheza Michezo ya Olimpiki huko Brazil mwakani, yameanza leo katika ufukwe wa hoteli ya Mbalamwezi Mikocheni Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha wenyeji Tanzania, Burundi na Kenya, Tanzania inashirikisha jumla ya timu nne, mbili za wanawake na mbili za wanaume.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo kwa upande wa akina dada, Tanzania iliibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya wenzao wa Burundi.
 
Timu hiyo namba moja ya Tanzania iliongozwa na Everlyine Alberth na Hellen Richard, tangu mwanzo ilionekana kuwazidi mbinu akina dada wa Kirundi Berth Mutoni na Janeth Kamwewe baada ya kuibuka na ushindi wa 21-17 katika seti ya kwanza.
 
Katika seti ya pili, Watanzania hao ambao timu yao inadhanimiwa na kinywaji cha Black Energy, waliongeza kasi na kuibuka na ushindi wa 21-16.


Wachezaji Hellen Richard (kushoto) na Everlyine Alberth kabla ya kuanza mchezo wao dhidi ya wenzao wa Burundi.
Hatahivyo, wanaume wa Tanzania walianza vibaya baada ya timu yao namba moja kushindwa kwa tabu na Burundi ambao ni mabingwa wa dunia kwa vijana wenye umri wa miaka 21 baada ta kufungwa seti 2-1.

Wachezaji wa Burundi Briand Mugabowingabo na Yvan Dukundane, ambao ni mabingwa wa dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, walishinda seti ya kwanza nay a tatu kwa 21-15 na 15-8 wakati Tanzania ilishinda seti ya pili kwa 21-19.


Mchezaji wa Tanzania Hellen Richard,
Timu namba moja ya Tanzania ilikuwa na wachezaji wa Karafuu ya Zanzibar Mohamed Ismail na  Farahan Aboubakar ambao walicheza vizuri muda wote wa mchezo lakini bahati haikuwa yao.

Mashindano hayo ambayo yanamalizika kesho yanashirikisha wenyeji Tanzania, Burundi na Kenya baada ya Djibout, Ethiopia na Somalia kutofika licha ya baadhi yao kuthibitisha kushiriki.



Kocha wa timu za taifa za Tanzania za mpira wa wavu Nasor Seif (kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wa timu ya pili  inayoshiriki mashindano ya wavu wa ufukweni ya Kanda ya Tano ya Afrika.
Wachezaji wa timu ya Tanzania na Burundi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo wao leo.
Tanzania na Burudi wakichuana leo katika ufunguzi wa Beach Volleyball leo

No comments:

Post a Comment