Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchujo ya ndondi za ridhaa yaliyopangwa kuanza leo
Jumatatu kwenye Uwaja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam, yameahirishwa,
imeelezwa.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT) Makoye Mashaga
alisema kuwa ukosefu wa fedha ndio umewafanya kuyasogeza mbele mashindano hayo.
Aliwataka wadau mbalimbali wa michezo na ndondi kujitokeza
kusaidia kudhamini mashindano hayo ili kuhakikisha yanafanyika kwa ufanisi
mkubwa ilikupata timu bora ya taifa.
Alisema mashindano hayo yatashirikisha jumla ya mabondia 39 lakini
watachujwa na kubaki 15 tu ambao wataingia kambini kwa ajili ya kujiandaa kwa
michezo hiyo ya Afrika itakayofanyika Brazzaville, Kongo Septemba mwaka huu.
MABONDIA
AMBAO WATASHIRIKI MCHUJO HUO:-
Lightfly: Ibrahim
Abdallah (Magereza), Said Hofu (JKT), Gervas Longasian (Arusha), Said Stephen
(Kigoma).
Fly: Shabani Mnimba
(Temeke), Hafidh Mohamed (JKT), Muhsin Kimwaga (JKT), Michael Andrew (Temeke).
Bantam: Tuwer Son
(JKT), James Star (JKT), Ahmed Furahisha (JKT), Bashir Mkumbula (JKT), Robert
Nobert (Kagera), Hassan Yussuf (Magereza).
Light: Bosco Bakari
(JKT), Swahiba Athumani (Arusha), Mohamed Ibrahim (Tanga) na Undule Langson
(Magereza), Fidel Castro (Kigoma) na Silaji Kassim (Kagera).
Walter: Victor
Njaiti (JKT), Issa Rashid (JKT), Shaban Bruno (Arusha), Kassim Khalfan (JKT) na
Babu Buluda (Morogoro).
Lightmiddle: Gulash
Rashid (JKT), Seleman Bamtula (JKT) na Mustapha
Mtoro (Temeke).
Middle: Ivan Mussa
(Kagera), Abuu Said (JKT), Hafidh Mwaipaja (Magereza), Frank Florian (Kigoma).
Lightheavy: Robert
Kyaruz (Kagera), Frank Kawesi (Lindi), Freddy Julius (Kigoma) na Daniel
Mwambinga (Magereza).
Heavy: Alex Sitta,
Maulid Kitenge na Fabian Gaudence.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment