Monday 9 February 2015

Uchaguzi kufanyika Nigeria-Serikali




LAGOS, Nigeria
WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Nigeria anaamini kuwa mapambano dhidi ya Boko Haram yatafanikiwa na uchaguzi huo utafanyika, imeelezwa.
Abbo Moro (pichani kulia) alisema kuwa amehakishiwa na jeshi kuwa, kutakuwepo na vikosi vya kutosha ndani ya wiki sita na uchaguzi huo utafanyika kwa usalama.
Viongozi wa Tume ya Uchaguzi walikaririwa wakisema kuwa uchaguzi huo wameuahirisha hadi Machi 28 kwa sababu vikosi vingi vya kijeshi vinavyohitajika kwa sasa vinapambana na askari wa Boko Haram.
Mgombea wa kiti cha urais kutoka upinzani Muhammadu Buhari ametaka kuwepo kwa utulivu na alipinga hatua hiyo ya kuusogezwa mbele uchaguzi huo.
Lakini alisema uhuru wa Tume ya Uchaguzi ya Nigeria umezikwa kutokana na uamuzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Wakati huohuo, Boko Haram imefanya uvamizi watatu kwa nchi jirani ya Niger, wakilenga mji wa Diffa uliopo mpakani. Mtu mmoja inadaiwa kuwa amekufa katika mlipuko huo wa bomu katika soko la mji huo.
Uamuzi wa Jumamosi wa kuahirisha kufanyika kwa uchaguzi huo mkuu ulipokewa kwa shangwe na chama tawala kinachoongozwa na rais Gooluck Jonathan ambaye naye anagombea, huku Marekani ikilaani na kusema imekatishwa tama na kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa ubunge ambao nao ulitakiwa kufanyika Februaru 28 sasa utafanyika Machi 28, na uchaguzi wa magavana wenyewe utafanyika Aprili 11.
Matukio Muhimu:
Januari 8: Rais Jonathan alizindua kampeni zake za urais.
Januari 14:Askati wa Boko Haram walivamia mji wa Biu uliopo Kaskazini- Mashariki ya Borno
Januari 18: Bomu liliua watu wane baada ya kuwekwa katika gari lililoegeshwa katika kituo cha basi huko Yobe.
Januari 25: Askari walivamia huko Kaskazini-Mashariki ya Maiduguri, huku watu kibao wakiuawa.
Februari 4: Boko Haram waliua watu hadi 70 baada ya kuvamia Cameroon.
Februari 6-8: uvamizi ulifanywa Niger.

No comments:

Post a Comment