*Aamini kama wameitoa Ghana kwa penati 9-8 katika fainali
Nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure baada ya kukabidhiwa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Ghana kwa penati |
MALABA, Guinea ya Ikweta
KIUNGO wa Ivory Coast na Manchester City Yaya Toure anaelezea
kushinda taji la Mataifa ya Afrika kama ni `kitu asichoamini’ baada ya Tembo kuwafunga Ghana `The
Black Stars’ kwa mikwaju
ya penati.
Kipa Boubacar Barry alifunga penati muhimu na kuifanya Ivory Coast
kushinda kwa penati 9-8 baada ya mchezo huo wa fainali kumalizika kwa suluhu
katika dakika 120.
Toure, aliyeshinda taji la Ligi Kuu ya England akiwa na Manchester
City msimu uliopita, alisema: "Unaposhinda ukiwa na kalbu yako, ni furaha
ya aina yake.
"Unapotwaa taji na nchi yako, ni kitu ambacho sikukitarajia."
Ivory Coast ilipata mafanikio pekee mwaka 1992, wakati ilipotwaa
taji hilo walipocheza tena na Ghana katika fainali na kuwafunga tena kwa
penati.
Mwaka huo, Ivory Coast ilishinda kwa penati 11-10 baada ya sare ya
kutofungana, lakini Barry aliokoa penati kibao wakati uo.
Wakati wa kupigiana penati, Barry kwanza aliokoa mchomo wa penati
uliopigwa na kipa mwenzake Brimah Razak kabla hajafunga penati ya ushindi
katika mchezo huo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Bata nchini Guinea ya
Ikweta.
Naye kocha wa timu hiyo Herve Renard aliweka historia, baada ya
kuwa kocha wa kwanza kutwaa mara mbili taji la Mataifa ya Afrika akiwa na nchi
mbili tofauti, kufuatia kutwaa taji na Zambia mwaka 2012.
"Bila kocha tusingeshinda taji, " aliongeza Toure, ambaye
ni nahodha wa Ivory Coast.
Kushindwa kwa Ghana kocha Avram Grant kunamkumbusha mwaka 2008 wakati
wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Chelsea ilipotolewa kwa
penati 6-5 na Manchester United, huku John Terry akiteleza na mpira wake kugonga
mwamba alipopiga mpira.
No comments:
Post a Comment