*Ni hofu ya Boko Haramu
LAGOS,
Nigeria
NIGERIA
imeahirisha kwa wiki sita uchaguzi wake mkuu wa rais uliopangwa kufanyika
Jumamosi kwa sababu ya hofu ya kiusalama. Imeelezwa.
Kiongozi
wa Kamisheni ya Uchaguzi ya Nigeria Attahiru Jega (pichani) alisema uchaguzi huo mkuu
umeahirishwa hadi Machi 28 na ilikuwa muhimu kufanya hivyo kwa sababu ya
kutokuwepo kwa vikosi vya ulinzi vya kutosha kwa ajili ya kuwalinda wapiga
kura.
Jeshi
la Nigeria limekuwa likipigana na wapiganaji wa Boko Haram huko
kaskazini-mashariki ya nchi.
Hatahivyo,
vyama vya upinzani vimesema kuwa kitendo hcho cha kuahirisha kwa uchagui huo ni
kurudisha nyuma demokrasia ya Nigeria.
Kiongozi
wazamani wa kijeshi Muhammadu Buhari, kutoka chama cha All Progressives
Congress (APC) anapambana na rais aliyemadarakani Goodluck Jonathan, anayeongoza
chama cha People's Democratic Party (PDP).
Habari
zinasema kuwa hadi uchaguzi huo unaahirishwa mchuano ulikuwa mkali kati ya
viongozi hao wawili.
Bwana
Jega jana Jumamosi alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Alisema
kuwa hatua aliyoichukua ni muhimu kwani alieleza kuwa vikosi vya usalama
havitakuwepo kusaidia wakati huo wa uchaguzi kwani viko katika zoezi maalum la
kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
"Kamishemi
ya uchaguzi kamwe haiwezi kupuuza ushauri wa kiongozi wa usalama wa nchi, "
alisema bwana Jega.
"Kuwaita
watu kutekeleza haki yao ya kidemokrasia katika hali isiyo ya kiusalama ni
suala lisilofaa kabisa.”
Hatahivyo,
viongozi kutoka APC wamelaani hatua hiyo ya kusogeza mbele uchaguzi huo wakidai
kuwa hatua hiyo ni kutaka kusaidia kampeni za rais aliyopo madarakani.
Mwenyekiti
wa APC John Odigie-Oyegun alisema kitendo hicho cha kuahirisha uchagui huo ni “pigo kubwa kwa demokrasia ya Nigeria ".
No comments:
Post a Comment