Sunday, 22 February 2015

Mwadui mabingwa Daraja la Kwanza

Kocha Mkuu wa Mwadui ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo `Julio' (kulia).
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Mwandui ya Shinyanga imefanya kweli na kuthibitisha kuwa haikubebwa katika Ligi Daraja la Kwanza na kufanikiwa kucheza Ligi Kuu baada ya kutawazwa mabingwa wa ligi hiyo.
Mwadui inayonolewa na Jamhuri kihwelo `Julio ilitawazwa kuwa bigwa wa Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuichapa African Sports ya Tanga kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex.
Bao hilo pekee lililokata ngebe za African Sports na kumuacha Julio akiendeleza tambo, liliwekwa kimiani na Kasika Kiduku kwa kichwa na kuwapa ubingwa Mwadui walioongoza katika kundi lao katika Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara Kundi B.
Mbali na Mwadui, nyingine zilizopanda kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao ni pamoja na Africans Sports ya Tanga, Toto Africans ya Mwanza na Majimaji ya Songea.

No comments:

Post a Comment