Wednesday, 18 February 2015

Blatter alaani ubaguzi wa Chelsea

Rais wa Fifa,Sepp-Blatter.
PARIS, Ufaransa
RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Soka Sepp Blatter amewalaumu mashabiki wa klabu ya Chelsea kwa kumzuia mtu mweusi kuingia ndani ya treni huku wakiimba nyimbo za kibaguzi jijini hapa.
Blatter amelaaini kitendo hicho kilichofanywa na baadhi ya mashabiki hao wa Chelsea cha ubaguzi wa rangi dhidi ya mtu huyo mweusi na kumzuia kuingia katika treni jana Jumanne.
Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wameonekana katika mkanda wa video wakizuia mlango wa treni kabla hawajamsukuma mtu huyo huku wakiimba nyimbo za kibaguzi: "Sisi wabaguzi, sisi wabaguzi na hicho ndicho tunachokitaka."
Tukio hilo lilitokea baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya uliofanyika jijini hapa na Chelsea kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Paris Saint-Germain kwenye uwanja wa Parc des Princes, huku klabu hiyo ikijibu haraka kuwa kitendo hicho sio cha kiungwana.
Ni wiki moja tu baada ya kocha wazamani wa AC Milan Milan Arrigo Sacchi kutoa kauli kuwa "kuna weusi wengi" katika ligi ya vijana ya Italia, ambapo Blatter akijibu matukio yote hayo katika mtanda wake wa kijamii wa Twitter.

No comments:

Post a Comment