Thursday, 26 February 2015

Atishiwa kuuawa baada ya kukosa penati





BELGRADE, Serbia
MCHEZAJI wa Serbian Zarko Udovicic (pichani),alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa kuuawa na mashabiki wa timu hiyo baada ya mchezaji huyo kukosa penati, kimesema Chama cha Wacheza soka wa kulipwa (FIFPro).
Beki huyo wa timu ya Novi Pazar alipaisha penati yake juu ya goli wiki iliyopita  katika Ligi Kuu ya Serbia dhidi ya FK Rad.
Siku mbili baadae, watu kadhaa walivunja chumba cha kubadilishia nguo kilichopo katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo katika klabu hiyo na kumuwekea bundiki usoni, ilisema taarifa hiyo ya FIFPro.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ndio alikuwa ameripoti tangu aondoke katika klabu hiyo ya Superliga.
Udovicic alikosa penati yake katika dakika ya 85 na FK Rad walishinda mchezo huo kwa bao 1-0.
Taarifa ya FIFPro ilisema: "Kama mfanyakazi yeyote, kila mtu anatakiwa kufanya kazi katika mazingira ya usalama. Sasa ni jukumu la soka na Serikali kuweka mazingira ya usalama kwa mchezaji huy."

Mirko Poledica, rais wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini serbia Nezavisnost, alisema Chama cha Soka cha Serbia na ligi havijachukua hatua yeyote.
"Lazima tusubiri hadi wafanya fujo michezoni wamuue mmoja wa wachezaji wetu? alisema.
"Kitu ambacho kinaniogopesa mimi ni kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na chama cha soka. Wameendelea kukaa kimya kabisa.
"Wanatakiwa wafanye kiti fulani ili kuwahakikishia wachezaji usalama. Lakini hawajafanya hivyo. Wakati mwingine mchezaji atauawa."

No comments:

Post a Comment