Thursday, 5 February 2015

Mancini awaponda wachezaji wakeKocha Roberto Mancini
MILAN, Italia
KOCHA Mkuu wa timu ya Inter Milan Roberto Mancini amewatupia lawama wachezaji wake na kuwafananisha na kuku baada ya kupoteza mchezo wa robo fainali ya Coppa nchini Italia dhidi ya Napoli.

Bao lililofungwa katika dakika za majeruhi na Gonzalo Higuain, lilitosha kabisa kuivusha Napoli kucheza nusu fainali ya mashindano hayo.

Mshambuliaji huyo Muargentina alitumia makosa ya beki wa Inter Andrea Ranocchia kufunga bao la ushindi baada ya kuujaza mpira pembeni kabisa ya lango.

Kipigo hicho ni cha tatu mfululizo kwa kikosi cha kocha Mancini.
Napoli, inayofundishwa na kocha wazamani wa Liverpool Rafael Benitez, sasa itakumbana na Lazio katika mechi mbili za nusu fainali.

"Huwezi kuruhusu kufungwa bao kama lile. Nimeshtushwa sana, "alisema Mancini (pichani).

"Muda wote tulicheza vizuri sana na tulikuwa kama timu, lakini huwezi kuruhusu kufanya makosa mengi namna ile. Kila tunapokwenda tunaruhusu mpinzani kufunga bao kirahisi.

"Tulikuwa mbali na Higuain ni mchezaji mzuriTulikuwa kama kundi la vifaranga vya kuku, alikuwa mmoja dhidi ya wachezaji watano. Ni bao la kizembe kuliruhusu. "

No comments:

Post a Comment