Monday, 9 February 2015

`Pearson bado kocha Leister City'

Kocha wa Leicester City Nigel Pearson
LONDON, England
UONGOZI wa timu ya Leicester City inayoshika mkia imekanusha taarifa kuwa umemtimua kocha wao Nigel Pearson.
Taarifa za vyombo vya habari zilizoripotiwa Jumapili usiku kuwa, klabu hiyo imemtimua kocha wao huyo mwenye umri wa miaka 51 baada ya timu hiyo kufungwa nyumbani na Crystal Palace, ikiwa ni kipigo chao cha tatu mfululizo na ni cha 15 katika msimu huu.
Lakini taarifa ya klabu ilisema Pearson anaendelea kuwa kocha wa klabu hiyo ya East Midlands.
"Taarifa kuwa tumetimua kocha hazina ukweli wowote na wala sio za msingi, alisema.
"Nigel, bado ni mfanyakazi na ni kocha wa kikosi cha kwanza na kwa sasa tunaangalia mchezo wetu wa Jumanne dhidi ya Arsenal nab ado juhudi zetu ni kucheza Ligi Kuu."
Jumamosi kocha huyo alimkaba mchezaji wa Palace, James McArthur.
Pearson, ambaye awali alikuwa akiifundisha Foxes kuanzia mwaka 2008-2010,amekuwa akiifundisha timu hiyo kuanzia Novemba 2011.

No comments:

Post a Comment