Sunday, 15 February 2015

Timu za A. Mashariki zang'ara Afrika

Kikosi cha Azam FC.
Na Mwandishi Wetu
TIMU za Afrika Mashariki zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Mabigwa wa Afrika zimeanza vizuri baada ya zote kushinda mechi zao za mwanzo.
Sasa timu hiyo zinasubiri mechi za marudiano ili ziweze kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kungara mwishoni mwa wiki.
Kwa Tanzania, Azam FC ambayo inashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza, jana Jumapili iliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya EL Merreikh ya Sudan katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Mbagala Chamazi.
Huko Kenya; wawakilishi wao katika mashindano hayo ya Afrika Gori Mahia iliibuka kifua mbele licha ya kupata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya CNaPS Sport ya Madagascar yenye naskani yake huko Miarinarivo.
Kutoka Uganda; wawakilishi wan chi hiyo katika mashindano hayo timu ya Kampala CCA   nayo iliutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 kutoka kwa Cosmos de Bafia ya Cameroon.
Sawa na Azam FC, Gori Mahia na wawakilishi wa Uganda wote walikuwa wenyeji wa mechi zao hizo na walicheza katika viwanja vyao vya nyumbani.
Katika mechi zingine mwishoni mwa wiki Kaizer Chiefs iliibuka na ushindi wa 2 1 dhidi ya Township Rollers katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa FNB.
Katika mchezo mwingine; Kaloum Star waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sewe Sport, Kano Pillars iliifunga Al-Malakia 2-0.
Nayo St Mitchel United ilitoka sare ya kufungana bao 1 1 na Mamelodi Sundowns.
San Pedro ya Ivory Coast ilipata kipigo cha kushtua wakati timu za Afrika Kusini za Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns zilijitutumua.
Sewe, klabu ya jeshi inayokuja juu barani Afrika ambayo haikuwa na bahati baada ya kushindwa na timu ya Misri ya Al-Ahly katika fainali ya Kombe la washindi mwaka jana, mwishoni mwa wiki iliteleza nyumbani baada ya kufungwa 2-1 na timu ya Guinea ya Kaloum.

No comments:

Post a Comment