MADRID, Hispania
KOCHA wazamani wa Manchester United David Moyes amekiri kuwa,
alipiga marufuku wachezaji wake kula chips wakati akifundisha klabu hiyo yenye
maskani yake Old Trafford.
David Moyes alisema kuwa alizuia wachezaji wake kula chips kwa
sababu alihisi baadhi yao waliongezeka uzito kutokana na kupenda kula chakula
hicho.
Moyes alikosolewa kufuatia kutimuliwa kwake Aprili mwaka jana,
huku Rio Ferdinand ambaye ni beki wa kati wazamani wa Man United akikosoa
uamuzi wa kocha huyo Mscotland wa kuzuia msosi huo kwa wachezaji wa timu hiyo.
Ulaji wa chips ulikuwa wa kawaida sana wakati wa kipindi cha kocha
Alex Ferguson aliyemtangulia Moyes hapo Manchester.
Moyes kwa sasa anafundisha timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania
ya La Liga ya Real Sociedad alifunguka kuhusu sababu za kupiga marufuku ulaji
wa chips alipokuwa Manchester United.
Kocha huyo alidai katika mahojiano na gazeti la Four Four Two kuwa,
baadhi ya wachezaji walikuwa vibonge.
“Ndio,
nilizuia ulaji wa chips," alisema Moyes, ambaye alifundisha kwa miezi sita
tu katika mkataba wake wa miaka sita pale Man United.
"Kwa sababu wachezaji baadhi ya wachezaji walikuwa vibonge na
sikufikiri kama chips ulikuwa mlo mzuri kwao."
Moyes pia alikiri kuwa hakufurahishwa na mapokezi aliyapata wakati
Man United waliposafiri kwenda Goodison Park katika msimu wa mwaka 2013-14.
Baada ya miaka 11 ya kuifundisha Everton, Moyes alirejea na
kupokewa kwa kuzomewa huko Merseyside wakati Man United ikichapwa 2-0 dhidi ya
klabu yake hiyo ya zamani.
Moyes, aliyetimuliwa baada ya kipigo hicho, alisema: "Sikushtushwa,
kwa sababu najua jinsi mashabiki walivyo na niliwaachia klabu yao. Lakini
nilisikitika sana kwa kitendo kile.
No comments:
Post a Comment