Saturday 7 February 2015

Zidane kumrithi Ancelotti Real Madrid




MADRID, Hispania
ZINEDINE Zidane ananolewa kuwa kocha ajaye wa klabu ya Real Madrid, alisema Carlo Ancelotti.
Zidane, ambaye kwa sasa ndiye anakinoa kikosi cha akiba cha Real Madrid cha Castilla, "ana viwango vyote " vinavyohitajika kushika usukani wa klabu, alisema Ancelotti alipozungumza na waandishi wa habari.
"Nafurahia kazi ya Zidane, anafanya vizuri sana, " alisema Ancelotti katika mahojiano hayo.
Baada ya mwanzo mgumu wa msimu, Castilla wako kileleni mwa ligi daraja la tatu ya Hispania.
"Anafanya vizuri sana katika mwaka wake wa kwanza wa kuifundisha timu hiyo. Ameichukua Castilla hadi katika nafasi ya kwanza na anatakiwa kuendeleza kazi hiyo nzuri.
"Kwangu ni wazi kuwa ana vigezo vyote vya kuwa kocha wa kuifundisha timu kubwa. Na ikiwemo Real Madrid," alisema kocha huyo Muitalia, aliyemteua gwiji huyo Mfaransa msimu uliopita.
Baada ya kushuhudia Castilla ikipoteza mechi zake tano kati ya sita za mwanzo, Zidane alibadili mambo na pamoja na ugeni wake katika kuifundisha timu hiyo, sasa amepoteza mchezo mmoja tu katika miezi minne iliyopita.
Timu hiyo inaweza kuongeza tofauti ya pointi endapo Jumapili kesho itashinda itakapocheza dhidi ya Athletic Bilbao.

No comments:

Post a Comment