Tuesday, 24 February 2015

Mwalimu afungiwa maisha baada ya kula uroda na mwanafunzi wake aliyemzidi miaka sita*Alimfuata hata alipomaliza shule na kujiunga na Chuo Kikuu

 
LONDON, England
MWALIMU wakike mwenye umri wa miaka 25, aliyekuwa akifanya ngono na mwanafunzi wake katika shule ya bweni, ambako alikuwa akifanya kazi, amefungiwa kufundisha.

Mwalimu huyo Ruth Vaughan (pichani),alikuwa `akichepuka na mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 18 wa shule ya Oakham.
Inaelezwa kuwa mwalimu huyo aliendelea kuwa na uhusiano wa ngono na mwanafunzi huyo katika miezi iliyofuata.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mwalimu huyo kwa sasa ameondoka katika shule hiyo kubwa ya umma baada ya kufungiwa kufundisha kutokana na kitendo chake hicho cha utovu wa nidhamu.
Mwalimu huyo kijana anayedaiwa `kutoka na mwanafunzi huyo katika shule hiyo ya bweni ambayo kwa mwaka inalipiwa kiasi cha pauni 30,000, inaelezwa kuwa, amefungiwa maisha kufundisha.
Dada huyo aliendelea `kutoka na mwanafunzi huyo ambaye amemzidi miaka sita, licha ya mwanafunzi huyo kumaliza shule hiyo, ambapo alikuwa akimtembelea mwanafunzi huyo wakati wa wiki yake ya pili Chuo Kikuu na kuendelea kufanya naye ngono huko huko chuoni.
Katika mahakama ambayo ilimtuhumu mwalimu huyo kutumia nafasi yake vibaya kwa kujiingiza katika mahusiano na mwanafunzi huyo licha ya mwanafunzi huyo kumaliza shule lakini alizidi kumfuata chuoni hapo na kuendelea kubinjuka naye.
Vaughan, 25, alikuwa mwalimu wa ubinifu na teknolojia katika shule ya Oakham huko Rutland, alihitimu katika vyuo na taasisi mbalimbali.
Mwanafunzi huyo amnaye alipewa jina la bandia la `Mwanafunzi A katika kesi hiyo, aliiambia mahakama hiyo huko Coventry kuwa, yeye na Vaughan walibusiana na kuachiana namba za simu mwaka 2013, ikiwa ni chini ya mwaka mmoja baada ya mwalimu huyo kuanza kufundisha shule ya Oakham.
Kijana huyo alisema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi katika kipindi chote cha majira ya joto ya mwaka huo wakati Vaughan alisisitiza kuwa wawili hao hawakufanya ngono hadi agosti 2013.
 

No comments:

Post a Comment