Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini |
LONDON,
England
KOCHA
wa Manchester City Manuel Pellegrini amekiri kuwa kikosi chake lazima
kijiimarishe zaidi baada ya kutoka sare ya 1-1 na Hull City katika mchezo wa
Ligi Kuu ya England.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu walihitaji bao la dakika za mwisho lililotokana na mpira wa
adhabu uliopigwa na James Milner na kuzuia timu hiyo kupata kipigo cha tatu
mfululizo baada ya David Meyler kuifungia Hull bao la kuongoza katika kipindi
cha kwanza.
Hatahivyo,
City, sasa wana pointi saba nyuma ya Chelsea, ambapo sasa inakabiliwa na
kibarua kigumu kutetea taji lake hiyo na imeshinda moja kati ya mechi sita za
Ligi Kuu, huku vinara wa ligi wakishinda 2-1 huko Aston Villa na kujiimarisha
uongozi wao kileleni.
“Lazima kujiimarisha
zaidi kwa sababu timu inacheza na wachezaji 10 na pamoja na yote
hatukutengeneza nafasi wala kufunga, ” alisema
Pellegrini. “Kila
pointi unayopoteza ni ngumu kuipata; kurejesha pointi saba ni ngumu sana zaidi
ya tano lakini huwezi kujua.
“Kwa kweli hatufikirii
kabisa kuhusu Chelsea, wanaoongoza kwa pointi saba katika msimamo wa ligi
lakini nao pia wanaweza kupoteza mchezo.
Muhimu zaidi kwetu ni kuimrisha safu yetu ya ushambuliaji.”
Mabingwa
hao watetezi walijitahidi wakitoana jasho na Hull City wakati wakishindwa
kuibuka na ushindi kwa mara ya tano katika mashindano yote.
“Tulimiliki mpira zaidi.
Tulifanya kazi ya ziada, tulikimbia, na kuchukua mipira, lakini inahitaji
mipango unapocheza na timu kama Hull,
Middlesbrough au Arsenal ambao watakuja hapa na wachezaji tisa au 10 nyuma ya
mpira, ” alisema Pellegrini.
“Inachanganya kwa sababu
timu ilifanya kazi wakati wote wa mchezo. Tulicheza zaidi, tulifanya kila siku
na tulifanya kila kitu…, “ alisema.
Man
City itaongezewa nguvu na kurejea kwa Wilfried Bony na Yaya Toure baada ya
kumalizika kwa fainali za Mataifa ya Afrika wiki hii lakini Pellegrini aligoma kukilaumu
kikosi chake kwa kukosekana wachezaji hao.
“Watasaidia wakiwepo
lakini zaidi ya kuwafirikia wao kinachotakiwa ni kufikiria wachezaji wanaocheza
kwa sasa, ” aliongeza kocha huyo.
“Labda inatubidi kutafuta
njia nyingine ya kucheza. Ni vigumu kujua sababu moja ya kutofanya vizuri.”
No comments:
Post a Comment