Saturday, 7 February 2015

Chelsea yazidi kujichimbia kileleni *Baada ya Man City kushindwa kuifunga Hull CityLONDON, England
KLABU ya Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya Jumamosi kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Pamoja na Aston Villa kufungwa, lakini timu hiyo kama ilikuwa na bahati baada ya kufanikiwa kuondoa ukame wa kufunga mabao baada ya kushindwa kutingisha nyavu za wapinzani kwa takribani saa 11.
Wakati Chelsea wakijiongezea pointi tatu muhimu, wapinzani wao wa karibu Manchester City wenyewe Jumamosi walijikuta wakilazimshwa sare ya 1-1 na Hull City nyumbani
Sare hiyo ya Man City ina maana kuwa, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya England wamepunguzwa kasi ya kuifukuzia Chelsea katika mbio za ubingwa.
Bao la ushindi la Chelsea liliwekwa kimiani na Branislav Ivanovic (pichani) na kuihakikishia Chelsea kuondoka na pointizote tatu muhimu.
Villa, ambao hawajafunga bao hata moja katika ligi tangu Desemba 20, walijibu mapigo vizuri baada ya kujikuta wakiwa nyuma kwa bao lililofungwa na Eden Hazard.
Hatahivyo, Villa waligangamala na kusawzisha kupitia kwa Jores Okore aliyefunga kwa kichwa mara baada ya kuanza kwa kiindi cha pili cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment