LONDON, England
BINGWA wa Olimpiki Christine Ohuruogu amekosoa kauli ya rais wa
Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) kuwa, mchezo wa riadha
unakabiliwa na mgogoro mkubwa dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.
Rais huyo wa IAAF Lamine Diack alisema kuwa "alishtushwa"
na madai kuwa viongozi wa IAAF walitumika kulinda matumizi ya dawa hizo nchini
Russia.
"Ni viguu sana kuendeleza mchezo wetu wakati hajui
kinachoendelea, " alisema Ohuruogu.
Akizungumza BBC radio 5 Live, Ohuruogu alisema: "Nafikiri
aina hiyo ya kauli haitakiwi…”
Desemba, TV ya Ujerumani ilidai kuwa viongozi wa riadha wa Russia
walikubali malipo kutoka kwa wanariadha kugawa dawa hizo zilizopigwa marufuku
na kuzuia usifanyike upimaji.
Wote waliodaiwa sasa wanachunguzwa na Kamishenu ya Nidhami ya IAAF,
ambayo itaamua kama viongozi wa kamisheni ya Russia ya kuzuia matumizi ya dawa
hizo, walihusika katika hilo.
Lakini Diack, ambaye atamaliza muda wake wa uongozi Agosti mwaka
huu baada ya kukalia kiti hicho kwa takribani miaka 16 kama mtu mwenye nguvu
sana katika mchezo huo, alikanusha kama kuna mtu yeyote anayelindwa.
Kwa mara ya kwanza akifanya mahojiano hadharani katika vyombo vya
habari tangu kutolewa kwa tuhuma hizo, Diack alisema: "Ni mgogo mgumu
lakini tutauweka kando na kusafisha hali hii ya hewa."
Ohuruogu alifungiwa kukimbia kwa mwaka mmoja baada ya kushindwa
katika vipimo mara tatu kabla hajarejea na kutwaa medali ya dhahabu.
Pia mdada huyo alishinda medali ya Olimpiki yam bio za mita 400
katika Olimpiki ya Beijing meaka 2008 na kuwa Muingereza wa kwanza mwanamke
kushinda mara mbili katika mashindano ya dunia wakati alipotwaa dhahabu huko Moscow
mwaka 2013 na kuongeza katika taji lake la mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment