Saturday, 7 February 2015

Man City yapania kuipiku Chelsea England

Nahodha wa Man City Vicent Kompany akibeba taji la Ligi Kuu ya England.
LONDON, England
NAHODHA wa Manchester City Vincent Kompany anaamini kuwa uzoefu wa sasa wa mabingwa hao unaweza kuwasaidia kukwea kileleni katika kiti walichokalia Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.
City iliyopo katika nafasi ya pili leo itacheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City kwenye uwanja wa Etihad ikiwa pointi tano nyuma ya vinara Chelsea, ambao nao leo watakuwa ugenini dhidi ya Aston Villa.
Kikosi hicho cha kocha Manuel Pellegrini kilikuwa pointi moja nyuma ya Liverpool wakati zimebaki mechi mbili kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu.
Na Man City ilikuwa point inane nyuma ya Manchester United wakati zimebaki mechi sita kabla hawajatwaa taji la Ligi Kuu siku ya mwisho ya msimu wa mwaka 2011/12 wakiwa chini ya kocha wazamani wa timu hiyo Roberto Mancini.
"Hii ndio hali ya kawaida kwetu, alisema beki huyo wa kati Mbelgiji, ambaye alikuwa mchezaji muhimu wakati timu hiyo ilipotwaa taji hilo mara zote mbili.
"Kuwa pointi tano nyuma Januari au Februari ni jambo kubwa.
"Tunajisikia vizuri kuwa katika nafasi hiyo. Tumekuwa katika nafasi hiyo mara nyingi."

Huku Man United wakitawala misimu miwili iliyopita, Chelsea waliweza kufanya mambo kama Man City kama wapinzani wakubwa katika mbio za kuwania taji.
Man United wamekuwa wakipambana tangu kuondoka kwa Alex Ferguson mwaka 2013 na sio ama mbadala wake, David Moyes na Louis van Gaal, aliweza kuiweka timu hiyo katika mbio za ubingwa.

Ratiba Ligi Kuu ya England:
Leo Jumamosi Januari 07, 2015
Tottenham     v    Arsenal   (Saa 9:45 alasiri)
Man City  v    Hull City (Saa 12:00 jioni)
Villa     v    Chelsea   (Saa 12:00 jioni)
Swansea  v    Sunderland  (Saa 12:00 jioni)
QPR  v    Southampton (Saa 12:00 jioni)
Leicester     v    Palace (Saa 12:00 jioni)
Everton   v    Liverpool (Saa 2:30 usiku)
Jumapili, Februari 08, 2015:
Burnley   v    West Bromwich (Saa 9:00 alasiri) 
Newcastle v   Stoke City (Saa 11:05).
West Ham  v   Man United


No comments:

Post a Comment