*Kila mchezaji apata pesa na mjengo wa nguvu
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara na nahodha Yaya Toure. |
YAMOUSSOUKRO, Ivory Coast
RAIS wa Ivory Coast Alassane Ouattara jana alimwaga mapesa zaidi
ya dola za Marekani Milioni 3.4 ikiwa ni zawadi kwa timu ya taifa ya nchi hiyo
kutwaa taji la Mataifa ya Afrika.
Waziri wa Michezo alisema kuwa rais amefurahishwa sana na ushindi
wa timu hiyo na ndio maana akatoa kiasi hicho cha fedha.
Timu hiyo kutoka Afrika Magharibi iliifunga Ghana kwa penati 9-8
vbaada ya timu hizo kutoka suluhu katika muda wa kawaida na ule wa nyongeza
katika fainali huko Guinea ya Ikweta.
Hilo ni taji lao la pili la Afrika kulitwaa baada ya lile la mara
ya kwanza mwaka 1992.
Kocha Herve Renard alikaribishwa katika makazi ya rais jana na
Mfaransa huyo alipata bonasi ya dola za Marekani 129,000.
Kikosi chake cha wachezaji 23 kila mmoja alipewa nyumba yenye
thamani ya 52,000 pamoja na fedha taslimu zenye thamani hiyo, kwa mujibu wa
waziri wa michezo Alain Lobognon.
Shirikisho la Soka la Ivory Coast lilipewa kiasi cha dola za
Marekani 429 000, pamoja na
benchi la ufundi waligawana kiasi cha dola 520
000, na kufanya fedha zilizotolewa na rais kuwa ya jumla ya pauni Milioni 3.
"Ahsanteni sana, kwa mara nyingine tena Ivory Coast imeungana
tena, " alisema Ouattara.
Umati wa watu ulifurika katika uwanja wa Felix Houphouet-Boigny
jijini Abidjan, ambako wachezaji waliingia katika gari la wazi pamoja na rais
wa nchi hiyo.
Umati wa wananchi wa Ivory Coast ukisubiri timu yao. |
No comments:
Post a Comment