Friday 6 February 2015

Ulinzi waimarishwa fainali Afcon



 *Ni Ivory Coastal uso kwa uso na Ghana kesho Jumapili

*Leo Jumamosi ni DRC na Guinea ya Ikweta saa 1:00 usiku


Baadhi ya polisi wa  Guinea ya Ikweta wakituliza vurugu uwanjani.

MALABA, Guinea ya Ikweta
IMEAMRIWA ulinzi kuimarishwa zaidi wakati wa mchezo wa  fainali ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika kesho Jumapili kati ya Ivory Coast na Ghana huko mjini Bata.
"Tumeomba polisi zaidi na usalama kuimarishwa uwanjani, “alisema Mkurunzi wa Hhabari wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) Junior Binyam.
"Tunataka uwepo mkubwa wa polisi na watazamaji kuhakikishiwa usalama zaidi uwanjani."
Ombi hilo limetolewa baada ya vurugu kutokea wakati wa mchezo wa nusu fainali iliyofanyika mjini hapa Alhamisi na kushuhudia takribani watu 36 wakijeruhiwa, huku mmoja akiumia zaidi.
Mchezo kati ya wenyeji na Ghana, ambayo iliibuka na ushindi wa bao 3-0, ulisimama kwa zaidi ya dakika 30 karibu na mwisho huku huku mashabiki wakitupa vitu kwa timu pinzani, wakipinga maamuzi ya waamuzi.
Hatua za kuimarisha ulinzi huo imekuja wakati waandaaji wakiendelea kujaribu kuujaza mashabiki uwanjani huo wenye uwezo wa kubeba watu 35,000 ili kutengeneza mazingira bora kwa ajili ya fainali ya mashindano hayo.
Mara nyingi mashindano hayo yamekuwa na kawaida na kushindwa kujaza uwanja pale mchezo wa fainali unapokuwa auhusishi timu mwenyeji, ingawa mahudhurio katika michezo hiii ya Guinea ya Ikweta ni bora ukilinganisha na miaka mingine.
Wakati huohuo, timu ya Kongo DR leo itaumana na wenyeji Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu utakaofanyika kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
 

No comments:

Post a Comment