*Ni pambano lenye utajiri miubwa kuliko yote duniani
Floyd Mayweather(kushoto) katika moja ya mapambano yake. |
NEW YORK, Marekani
BONDIA Floyd Mayweather atapambana na Manny Pacquiao huko Las
Vegas Mei 2 katika pambana linalosemekana kuwa la utajiri mkubwa katika
historia ya ngumi za kulipwa duniani.
Mmarekani Mayweather, 37, ma Mfilipino Pacquiao, 36, wanafikiriwa
kuwa ndio mabondia wawili bora zaidi kwa sasa katika kipindi hiki.
Mayweather ni bingwa wa WBC na WBA wa uzito wa welter wakati Pacquiao
ni bingwa wa uzito huo wa WBO na watazichapa katika ukumbi wa MGM Grand.
Mayweather hajawahi kupigwa katika mapambano yake 47 aliyocheza
katika ndondi za kulipwa wakati Pacquiao ameshinda mara 57 na kupoteza
mapambano matano kati ya mapambano 64 aliyocheza.
Pambano hilo linatarajia kutengeneza kiasi cha Pauni Milioni 162 (sawa na dola Milioni 250). Likiwa pambano litakaloingiza
faida zaidi katika historia, ambapo inafikiriwa pambano la Mayweather dhidi ya Saul
Alvarez mwaka 2013, linadhaniwa liliingiza karibu pauni Milioni 97.
Pambano la Mayweather na Pacquiao pia linatarajiwa kuvunja rekodi
ya watazamaji wengi kuangalia katika TV ya kulipia.
Hadi sasa pambano ambalo liliingiza fedha nyingi kwa watazamaji
kulipia malipo ya TV ni lile la Mayweather alipopigana na Mmarekani mwenzake Oscar
de la Hoya mwaka 2007.
Mayweather aliandika katika ukurasa wake: "Kile ambacho dunia
ilikuwa ikikisubiri kwa muda mrefu hatimaye kimewadia, Mayweather vs Pacquiao Mei
2, 2015.
No comments:
Post a Comment