Thursday, 5 February 2015

Ivory Coast yatinga fainali kwa kishindo Afcon*Yaichapa Kongo DRC 3-1

 *Kocha hajaridhishwa na kiwango

Kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast.
MALABO, Equatorial Guinea
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast Herve Renard anafikiri timu yake inahitaji kuimarika zaidi ya vile ilivyoibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Kongo DRC katika mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Renard alisema kuwa endapo Ivory Coast inataka kumaliza ukame wa miaka 23 wa kutwaa taji hilo inawabidi kubadilika zaidi katika mchezo wa fainali Jumapili, ambao utawakutanjsha ama na Ghana au wenyeji Equatorial Guinea.

Nusu fainali ya pili inafanyika leo na inazikutanisha Ghana na Equatorial Guinea.

"Niwe mkweli kwenu, kwa kweli sikupendezwa na mchezo wenu, " alisema Renard,mwenye umri wa miaka 46."Nafikiri hatukufanya vyote tulivyotakiwa kuvifanya."

Kocha huyo Mfaransa aliongeza: "Nafikiri wakati fulani tulikuwa wepesi sana.

"Sasa tuko katika fainali, na hicho ndio kitu muhimu sana."

Yaya Toure ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia bao Ivory Coasta na kukiwezesha kikosi hicho cha Renard kuwa mbele, lakini Eric Dailly aliunawa mpira kusababisha Kongo kusawazisha kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na Dieumerci Mbokani.

Wakati kipute kikiendelea, Ivory Coast waliimarika zaidi na kupata mabao yaliyofungwa na washambukiaji wake Gervinho na Wilfried Kanon.
"Hii ni hatua moja mbele katika maisha yetu," alisema mshambuliaji wa Ivory Coast na Manchester City Wilfried Bony.

"Tunatakiwa kufurahia  usiku huu na kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumapili. Ulikuwa mchezo mgumu, kwani DR Congo walikuwa wakicheza kwa kasi lakini tulikuwa imara.

"Tunchofikiria sasa ni kurudi na taji nyumbani."

No comments:

Post a Comment