Saturday, 7 February 2015

Arsenal yakiona cha mtema kuni
LONDON, England
TIMU ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kuwafunga Arsenal kwa bao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Engand kwenye uwanja wao wa White Hart Lane Jumamosi.
Arsenal ndio walianza mchezo huo kwa kasi zaidi na kuonekana kama wangeibuka na ushindi na wakipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil (pichani) aliyefunga katika dakika ya 11,
Spurs walisawazisha  bao hilo kupitia kwa mshambuliaji chipukizi Harry Kane aliyefunga katika dakika ya 56 ikiwa ni dakika tisa tangu kuanza kwa kipindi cha pili.
Kane aliwahakikishia Tottenham pointi zote tatu kwenye dakika ya 86 kwa kufunga bao la pili na kuwapaisha hadi katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.
Kane hadi sasa amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo ambapo anashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa wafungaji wanaoongoza kwa kupachika mabao.
--
Matokeo ya mechi zingine za Ligi Kuu ya England zilizochezwa Jumamosi:
Queens Park Rangers   wamepokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Southampton huku Manchester City   ikilazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Hully Citi na Southampton ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutka kwa Swansea City 0 1.

No comments:

Post a Comment