Monday 30 April 2018

Simba Yauota Ubingwa Ligi Kuu Bara


Na Mwandishi Wetu
BAADA ya Simba kufanikiwa kuzoa pointi tatu kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao Yanga, kocha wa timu hiyo, Pierre Lechantre amejinadi kuwa, hakuna anachokisubiri sasa zaidi ya ubingwa.

Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuwafanya wazidi kujikita kileleni mwa msiamamo wa ligi wakiwa na pointi 62 wakiwaacha Yanga katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 48, lakini bado wana mechi mbili zaidi mkononi.

Simba ambao wamebakisha mechi nne wanahitaji pointi tano tu ili watangazwe kuwa mabingwa wa msimu huu kutokana na Yanga ambao wamebakiwa na michezo sita kuwa kama wakishinda mechi zao zote watakuwa wamefikisha pointi 66.

Akizungumza na gazeti hili kocha huyo raia wa Ufaransa alisema kuwa mchezo dhidi ya Yanga ulikuwa ukimnyima raha, kwani alikuwa akiupigia hesabu kali za kutaka kuondoka na pointi tatu.

Alisema alikuwa akiamini wazi kuwa kama atafanikiwa kuwafuinga mahasimu wao hao njia ya ubingwa kwao itakuwa nyeupe kutokana na pengo la pointi lililopo.

“Muda mrefu mlikuwa mkiniuliza kuhusu hii mechi lakini tumeshinda, niliwaambia wachezaji wangu tushindi hii mechi na baada ya kupata alama hizi tatu nina uhakika mkubwa sasa sisi ni mabingwa, tupo vizuri katika mahesabu ,” alisema Lechantre.

No comments:

Post a Comment