Tuesday 17 April 2018

Diamond Ashikiliwa na Polisi kwa Video `Chafu'


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe ameagiza kukamtwa kwa msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul au Diamond kutokana na video yake ya faragha iliyosambaa hivi karibuni.

Mwakyembe ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ulanga,Goodluck Mlingwa aliyehoji jinsi gani serikali imejipanga kupambana na wasanii wa muziki pamoja na vikundi vya watu wanaosambaza lugha za matusi.

Aidha, alisema msanii Diamond tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi kutokana na video yake ya faragha iliyosambaa akiwa kitandani na hamisa Mobetto.

"Wasanii wetu ambao walianza kufanya uhuni uhuni ndani ya mitandao ya kijamii tumeweza kumkamata  Diamond na tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha chafu alizozirusha," alisema Mwakyembe.

Kwa upande mwingine Waziri Mwakyembe amewaonya vijana kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii, ambapo alisema mitandao hiyo ni vyema ikatumika vizuri kwa masuala ya maendeleo na sio kuharibu utamaduni wetu.

No comments:

Post a Comment