Saturday 28 April 2018

Kuziona Simba, Yanga Zikiumana ni Buku Saba Tu


Na Mwandishi Wetu
KESHO jiji la Dar es Salaam na viunga vyake litazizima kufuatia mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga utakochezwa Uwanja wa Taifa, huku kingilio cha juu zaidi katika mchezo huo ni Sh 30,000 wakati cha chini ni 7,000, imeelezwa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliwambia waandishi wa habari jana kuwa tiketi za mchezo huo zinapatikana Celcom pamoja na mawakala kituo cha mafuta cha Total kilichopo Uhuru pamoja na Uwanja wa taifa.

Alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh 30,000 kwa VIP A, wakati VIP B ni Sh 20,000 huku mzunguko ikiwa ni Sh 7,000.

Akizungumzia mchezo huo Manara alisema: "Mchezo utakuwa mgumu, Yanga ni wakubwa wenzetu, tunawaheshimu, "alisema.

"Mashabiki wanataka ubingwa, matokeo ya mechi yetu na Yanga ndio yatakayotoa mustakabali wa ubingwa wetu, alisema  na kuongeza:

"Wachezaji wanajua nini tunataka, siwezi kusema lazima tushinde, mpira una matokeo matatu, kufunga, kufungwa na kutoka sare, mechi ndio itatoa mwelekeo wa ubingwa,"alisisitiza.

Simba na Yanga watashuka katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, katika mchezo wa marudiano utakaopingwa  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo katika mchezo wa kwanza timu hizo zilifungana 1-1.

Simba itashuka dimbani huku ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi Simba inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 24 huku Yanga ikiwa inaifukuza kwa nyuma kwa pointi 47 akiwa na amecheza mechi 23.

No comments:

Post a Comment