Friday 27 April 2018

Bill Cosby Atupwa Jela Miaka 10


NEW YORK, Marekani
MCHEKESHAJI mahiri wa Marekani Bill Cosby (pichani) amehukumiwa kwenda jela zaidi ya miaka 10 baad aya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha kijinsia mwanamke mmoja, Andrea Constand zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Msanii huyoi wa vichekesho alikutwa na hatia katika makosa matatu, ambapo sasa mashabiki wake, ambao walifurahia vichekesho `live’ kwa zaidi ya miongo minne, na sasa wataona skrini za sinema.

Cosby alikuwa pia akituhumiwa na zaidi ya wanawake wengine 50 kwa kuwanyanyasa kijinsia, lakini hawakumpeleka mahakamani na kuonekana hana hatia katika madai hayo.

Muigizaji huyo, mwenye umri wa miaka 80 sasa, alikuwa akituhumiwa kumnyanyasa kinjinsia mchezaji wazamani wa mpira wa kikapy Andrea Constand mwaka 2004.

Cosby,ambaye ni muigizaji wa kwanza mkubwa wa Kiafrika katika TV, ataendelea kuwa nje hadi pale hukumu yake itakavyothibitishwa.

Hatahivyo, wakili wake alisema kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo dhidi ya mteja wake.

Hii ilikuwa mara ya pili kwa muigizaji huyo kusimama mahakamani kwa shtaka kama hilo, lakini hakupatikana na hatia Juni mwaka 2017.

Cosby anajulikana sana kwa maonesho katika TV katika miaka ya 1980 iliyojulikana kama Cosby Show.

Mwanasheria wa Cosby, Tom Mesereau alisisitiza kuwa “mpambano bado unaendelea”, akiongeza kuwa anaamini Cosby hana hatia na ana mpango wa kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment